Lady Jaydee aelezea mahusiano yake na Spicy kwa sasa


Msanii wa muziki Bongo, Lady Jaydee amefunguka ni kwanini kwa sasa haonekani akimposti zaidi mpenzi wake Spicy.

Muimbaji huyo amesema kuwa mwanzo alikuwa akifanya hivyo kutokana walikuwa katika promotion ya wimbo wake ‘Together Remix’ ila kwa sasa mahusiano yao yanabaki kuwa binafsi zaidi.

“Watu wasisahau pia mimi ni Lady Jaydee na ile page ni ya Lady Jaydee sio page ya Spicy kwa hiyo mambo ya binafsi yanaendelea kubaki kuwa ya binafsi lakini kama kuna ulazima wa kitu chochote kufanya basi atapostiwa,” amesema.

“Ila sipendi kwenye masuala yangu binafsi iwe picha nyingine ya mtu mwingine kiasi kwamba huyo mtu asipoonekana kidogo watu wanaanza kuhoji ni kwanini, kwa maisha ya lady Jaydee kama msanii yataendelea kama Lady Jaydee na maisha yangu kama ya mapenzi, familia yataendelea kuwa kama yalivyo,” alisema Jide

Lady Jaydee amekuwa katika mahusiano na msanii mwenzake Spicy kutoka nchini Nigeria, pia wameweza kutoa ngoma pamoja ambayo remix ya ngoma ‘Together’ ambayo hapo awali aliimbia Spicy pekee yake. Pia Spicy ametokea katika video ya wimbo wa Lady Jaydee uitwao Baby.