KUELEKEA KOMBE LA DUNIA: IJUE SENEGAL

Na Eston Eston
Zikiwa zimebaki siku 13 kuelekea kombe la dunia macho ya wapenzi wote wa soka ulimwenguni pote yaamie nchini Urusi tunakuletea mtiririko mzuri wa makala za nchi shirikishi katika mashindano hayo makubwa zaidi katika ngazi zote za mashindano ya mpira wa miguu. Na leo tunaanza kwa kuangazia moja ya washiriki kutoka nyumbani barani Africa nao sio wengine ni Senegal.

Senegal ambao ukipenda unaweza waita “Simba wa Teranga” wanaelekea kwenye mashindano hayo tena baada ya miaka 16 tangu wafanye hivyo kwa mara ya mwisho mwaka 2002 wakiwa na kumbukumbu nzuri kwenye mashindano hayo ya kwanza kwao katika michuano hio walipofanikiwa kuwa timu ya 2 kutoka barani Africa kutinga robo fainali ya kombe la dunia baada ya miamba mingine ya Africa Cameroon kufanya hivyo miaka ya 1990.

Simba hao wa teranga wamerejea tena kwenye mashindano hayo na hawana sana tofauti na Senegal ile ya El Hadji Diouf na kina Henri Camara hii ya sasa imejaa mastaa wengi pia wanaotamba katika vilabu vikubwa barani Ulaya ,macho ya wasenegal na waafrica wote yatakuwa zaidi kwa staa wa Liverpool ya ya Uingereza Sadio Mane ambae amekuwa na msimu mzuri sana kwa mwaka huu ndani ya klabu yake yake Liverpoo na tayari ameshaifungia Senegal magoli 14 katika michezo 51 alioichezea Senegal mpaka sasa. Lakini pia kiungo wa Monaco anetarajia kuungana na Mane msimu ujao kunako Liverpool nae anatazamwa kama moja ya wachezaji muhimu ndani ya wana samba hao wa teranga. Si haba pia kwa upande wa safu ya ulinzi beki kisiki wa Napoli ya Italia Kalidou Koulibaly anatazamiwa kuingoza vema safu ya ulinzi ya timu hio.

Kwa ujumla kikosi kamili cha Senegal kinachonolewa na Aliou Cisse kimejaa mastaa wengi wanaokipiga katika ligi kubwa barani ulaya. Vilabu kama vile Liverpool,Everton,Westham,Stoke city,zote za nchini Uingereza lakini pia Napoli,Torino na Spal zote za nchini Italia,Bordeaux na Rennes pia kutoka Ufaransa na Hannover ya ujerumani. Wachezaji 23 wanaounda kikosi cha Senegal wengi wao wanatoka katika vilabu hivyo barani Ulaya.

Namna walivyofuzu,Senegal ilikuwa kundi D pamoja na Burkina Faso,Cape Verde pamoja na Afrika Kusini ilimaliza wa 1 katika kundi hilo bila kupoteza mechi yoyote baada ya kushinda michezo 4 na kutoka sare 2 na hivyo kujikatia tiketi moja kwa moja kuelekea Urusi wakiwaacha Burkina Faso nafasi ya pili kwa tofauti ya point 5 katika kundi hilo.

Mechi za karibuni, tangu wafanikiwe kufuzu kuelekea kombe la dunia nchini Urusi Senegal wamecheza michezo michache ya kirafiki kuhakikisha wanajiweka sawa kuelekea mashindano hayo. Marchi 23 walicheza na Uzbekistan wakatoka sare ya 1-1. Marchi 27 wakashuka dimbani tena kuvaana na Bosnia wakatoa sare nyingine ya bila kufungana na May 31 wakatoa sare yao ya


3 dhidi ya Luxembourg. Na wanatarajia kucheza mchezo wao wa mwisho wa kirafiki dhidi ya Croatia juni 8 kabla ya kuvaana na Poland juni 19 kwenye kombe la dunia.

Kundi walilopangwa, Senegal wamepangwa kundi H pamoja na timu ya Poland,Japan na Colombia. Mchezo wao wa kwanza utakuwa dhidi ya Poland juni 19 na juni 24 watakipiga na Japan kabla ya kumaliza na Colombia juni 28.

Matarajio, pamoja na kuwa na uzoefu mdogo kwenye mashindano hayo bado wasenegali wengi na waafrica kiujumla wana matumaini makubwa kwa simba hao wa teranga. Uzoefu wa wachezaji wao wengi wanaotamba kwenye ligi kubwa barani Ulaya na mchanganyiko mzuri wa wachezaji wakongwe na vijana unawapa nguvu na jeuri kuamini watafanya vema. Lakini mafanikio waliyovuna pia mwaka 2002 yanawapa matumaini kuamini watafanya vema tena kwa mara nyingine.

Kikosi kamili, Makipa:Khadim Ndiaye (Horoya AC), Abdoulaye Diallo (Rennes), Alfred Gomis (Torino)

Mabeki:Kara Mbodji (Anderlecht) Kalidou Koulibaly(Napoli), Moussa Wague (Eupen), Saliou Ciss (Angers), Youssouf Sabaly (Bordeaux), Lamine Gassama (Alanyaspor), Armand Traore (Nottingham Forest), Salif Sane (Hannover 96)

Viungo:Pape Alioune Ndiaye (Stoke) Idrissa Gueye (Everton),Cheikhou Kouyate (West Ham), Cheikh N’Doye (Birmingham)

Washambuliaji: Sadio Mane (Liverpool), Diao Balde Keita (Monaco), Ismaila Sarr (Rennes), Diafra Sakho (Rennes), Moussa Konate (Amiens), Mame Biram Diouf (Stoke), Mbaye Niang (AC Milan).

MaoniMaoni Yako