Kombe la dunia na vibweka tarajiwa

BangladeshMkulima mmoja mwenye asili ya Bangladeshi ameonesha uungaji mkono wa aina yake kwa timu ya Ujerumani inayoshiriki kombe la dunia kwa namna ambayo si ya kawaida, baada ya kutengeneza bendera yenye urefu wa kilomita 5.5 ama maili 3.4.
Mkulima huyo anaitwa Amjad Hossain, mwenye umri wa miaka 69, ameelezea mapenzi yake kwa nchi ya Ujerumani baada ya kutumia dawa kutoka nchini humo kutibu tatizo la homeopathic.
Amjad alianza zoezi la utengenezaji bendera hiyo miaka miwili baadaye, baada ya ujerumani kuwa mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia mnamo mwaka 2016, na imeendelea kuongezea katika mashindano yaliyo fuata.Hosain alidiriki kuuza hata ardhi aliyokuwa anaimiliki ili mradi tu anunue kitambaa cha kutosha,chenye rangi nyeusi, nyekundu na dhahabu.
Bangladesh
Bendera hiyo ilizinduliwa rasmi mapema wiki hii katika shule ambayo bwana Hossain kwenye mji alikozaliwa wa Magura, kama maili 60 sawa na kilomita mia moja upande wa kuelekea magharibi mwa mji mkuu Dhaka.
Kwa muujibu wa shirika la habari la AFP, Amjad anapanga kuionesha bendera hiyo katika viwanja vya kwao ikiwa Ujerumani itainfia nafasi ya pili katika michuano hiyo ya kombe la dunia na kusema kuwa anamapenzi ya dhati kwa timu hiyo.Amenukuliwa akisema analipenda soka la Ujerumani , wanatandaza kandanda murua .
Wakati wa michuano ya kombe la dunia la mwaka 2014, wakati bendera yake ilipokuwa na urefu wa kilomita 3.5 tu - balozi wa Ujerumani nchini Bangladeshi alimpa Amjad uanachama rasmi na wa maisha wa klabu ya taifa la Ujerumani na shabiki wa kudumu wa timu hiyo , akapewa pia mpira, jezi ya timu hiyo pamoja na cheti cha utambuzi.
by richard@spoti.co.tz