Kichuya azigomea M70 za Simba Azam yatajwaSTAA anayependwa na mashabiki wa Simba kutokana na uwezo wake wa kuzinyanyasa timu pinzani, Shiza Kichuya amegoma kuchukua Sh70milioni alizowekewa mezani ili aongeze mkataba mpya.


Kichuya ni kati ya wachezaji wa Simba ambao mikataba yao imemalizika msimu huu wa Ligi Kuu Bara akiwemo Said Ndemla, Mohamed Ibrahim, Mzamiru Yassin na Laudit Mavugo. Wakati Simba wakiendelea na mazungumzo ya kumuongezea mkataba Kichuya, Azam FC nayo

imeelezwa kuingia vitani ikitaka kumsajili kiungo huyo anayetumia mguu wa kushoto.


Kwa mujibu wa taarifa ambazo Championi Jumamosi imezipata zinasema, kiungo huyo akiwa na meneja wake, uongozi wa Simba walishindwa kufikia muafaka mzuri wa kumuongezea mkataba mpya kiungo huyo kutokana na dau kubwa analolitaka.


“Uongozi wa Simba bado unapambania jinsi ya kumsainisha Kichuya na hakuna kingine zaidi ya fedha pekee ambayo ndiyo imekwamisha kwani kuhusu mazungumzo ya awali tayari yamefanyika na mwenyewe ameonyesha nia ya kuongeza mkataba.


“Kama Kichuya akipatiwa fedha anayoihitaji tofauti ya shilingi milioni 70 aliyoikataa basi ata

saini mkataba, lakini tunashukuru mazungumzo yetu Simba na yeye mchezaji yanakwenda vizuri,” alisema mtoa taarifa huyo. Kaimu wa Rais wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ jana alizungumzia usajili wa Kichuya na kusema kuwa: “Wachezaji wetu wanne tupo kwenye mazungumzo nao kwa ajili ya kuongeza mkataba mwingine mpya, akiwemo Kichuya.” “Kichuya tupo kwenye mazungumzo naye mazuri ambayo tutayafikia muafaka hivi karibuni kwani yeye mwenyewe na meneja wake tulikutana na kujadiliana nao.


“Mchezaji huyo bado tunamuhitaji katika timu yetu kutokana

na mchango mkubwa alioutoa kwenye msimu huu wa ligi na kutuwezesha kutwaa ubingwa wa ligi,” alisema Abdallah.


“Hakuna mchezaji tunayemuhitaji tukashindwa kumsajili, kama uongozi tumepanga kumsajili mchezaji yeyote tutakayemuhitaji kutokana na mapendekezo ya kocha atakayoyatoa,” alimalizia Abdallah ambaye si mzungumzaji sana kwenye vyombo vya habari. Baba wa Kichuya alinukuliwa na Championi akimtaka mwanae asisaini mkataba kwa mazoea Simba bali aangalie masilahi yake na soko lake