Kamusoko aliamsha dude Kenya


Nakuru. Nahodha wa Yanga, Thaban Kamusoko anaamini timu yao iko vizuri kushindana dhidi ya Kakamega Homeboys kesho Jumapili ili kuweza kusonga mbele katika michuano ya SportPesa Super Cup.
Yanga inafungua dimba na Kakamega kesho mchana kabla ya Gor Mahia kumenyana na JKU ya Zanzibar baadaye jioni mechi zote zikiwa mbashara Startv.
"Tumejiandaa vizuri kucheza na Kakamega. Hatuwafahamu sana lakini wao wanaifahamu Yanga ni timu ya aina gani, wanatuona kwenye mashindano ya kimataifa, lakini hilo halitoshi kutuzuia tusipate ushindi," alisema Kamusoko.
Yanga inakwenda katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa mabao 3-1 na Azam katika mchezo wake wa mwisho wa Ligi Kuu Bara.
Bingwa wa mwaka huu ataondoka na kitita cha Ksh.3milioni na fursa ya kuifuata Everton ya England kwenye Uwanja wake wa Goodison Park.
Mshindi wa pili atavuna Sh 1 milioni huku washindi wa tatu na nne wakiondoka