Je Huu Ndo MJengo wa Aslay??

Hivi karibuni millardayo.com na Ayo Tv zilifanya mahojiano na muimbaji Aslay ambaye alisema kuwa pesa ya kubadilishia mboga anayo na ikiwemo gari yake aina ya BMW na nyumba ya kuishi, sasa leo June 2, 2018 mkali huyo kutokea bongoflevani ametuonesha picha za mjengo mkali na yeye akiepo.

Je hii ndo nyumba ya Aslay tunayoisikia…? millardayo.com inakukaribisha kutazama baadhi ya picha alizotuonesha mkali huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram…..>>>”Mambo Mawili Huonesha Picha Yako Halisi (1) Subila Yako Ukiwa Huna Kitu (2)Mwenendo Wako Pindi Unapokuwa Na Kitu, Kila Hatua Dua #dingimtoto“ – ASLAY