Himid Mao asajiliwa Misri


KIUNGO na nahodha wa Azam FC, Himid Mao, amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kujiunga na Petrojet ambayo inashiriki imid ambaye ameitumikia Azam FC kuanzia akiwa na timu ya vijana mwaka 2011, alisaini mkataba huyo juzi na atakuwa chini ya kocha mkongwe, Hassan Shehata.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Azam FC, Jaffar Idd, alisema kuwa nahodha huyo aliondoka nchini akiwa na baraka za klabu hiyo.
“Uongozi sisi hatuna kipingamizi, Himid ni mchezaji wetu wa muda mrefu tangu akiwa mdogo kabisa na ameshiriki mafanikio mengi ya timu, mara baada ya kuleta maombi hayo sisi tulimkubalia na tunamtakia kila la kheri huko aendako katika maisha yake mapya,” alisema Idd.
Licha ya kuondokewa na nahodha wao, Azam imeanza maandalizi ya kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao kwa kumtangaza, Mholanzi, Hans van der Pluijm kuwa ndiye kocha wake mpya na vile vile kumsajili mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma.
Mbali na kuipa mataji mbalimbali, Pluijm ambaye pia aliwahi kuifundisha Medeama ya Ghana ameisaidia Singida United kufika fainali ya Kombe la FA ndani ya msimu mmoja ambao ameifundisha.Ligi Kuu Misri, imefahamika.