Hatimaye Yaya Toure Ameamua Kufunguka Ukweli 'Pep Guardiola ni Kocha Mbaguzi'


Kiungo wa zamani wa club ya Man City ya England Yaya Toure ameamua kuvunja ukimya na kuzungumzia ishu iliyopo nyuma ya pazi kati yake na kocha Pep Guardiola ambaye mara kadhaa amewahi kuingia matatizoni na wakala wa Yaya Toure.

Toure ameamua kufunguka na kueleza kuwa kocha Pep Guardiola ana matatizo na wachezaji wa kiafrika, Toure ambaye ameichezea Man City kwa miaka nane toka alipojiunga nayo mwaka 2010 akiuzwa na Guardiola baada ya kuteuliwa kuwa kocha wa Barcelona.Yaya Toure ameeleza kuwa sio yeye pekee ndio mchezaji mweusi ambaye amewahi kumshuku Guardiola kuwa ana ubaguzi wapo wengi wakati anacheza Hispania amewahi kuwa na mvutano nao.

“Nataka kuwa mtu wa kwanza kueleza ukweli kuhusu Guardiola, nafikiri nilikuwa nafanya kazi na mtu ambaye ana mpango wa kulipiza kisasi kwangu, sijui ni kwa nini lakini nimekuwa na mawazo kuwa Guardiola ananionea wivu” Toure
“Nakuahidi siku ikitokea Pep Guardiola akapanga kikosi chake cha kwanza (first eleven) kikawa na wachezaji watano wakiafrika ukiacha waliopewa uraia wa Ulaya, nitampelekea keki”>>>Toure