Harmonize na Wolper uso kwa uso

Baada ya drama za hapa na pale hatimaye Harmonize na ex-girlfriend wake Jackline Wolper kukutana katika tukio moja.

Tukio hilo ni show ya Harmonize ‘Kusi Night’ itakayofanyika Dar Live siku ya Eid Pili June 17, 2018 ambapo Wolper atakuwa host wa show hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo June 05, 2018 Dar es Salaam, Harmonize amesema kuwa amemchangua Wolper kufanya hivyo ni kutokana anaweza hilo na kuonesha hakuna tofauti kati yao.

“Wolper ana uwezo wa ku-host show, kwa sababu ameshazoea sana mambo haya, pengine kwenye movie wako location, halafu pili kitu kingine Wolper ana fan base kubwa naamini ataweza kuisimamia show vizuri,” amesema.

“Lengo ni kuwaonesha watu kuwa hatuna tatizo mimi na yeye na tunashirikiana katika kazi, hii yote tunaepusha kuwagawa mashabiki, yeye ana mashabiki zake na mimi nina wangu,” amesisitiza.

Utakumbuka Harmonize na Wolper walikuwa katika bifu zito kitu kilichopelekea kutupiana maneno katika mitandao na kwenda mbali zaidi hadi kumuhusisha mpenzi wa sasa wa Harmonize, Sarah.