Fred kufanyiwa vipimo Wiki Hii Man United

Kiungo wa kimataifa wa Brazil, Frederico Santos maarufu kama Fred anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Manchester United wiki hii.

Fred anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya leo hii kabla ya kutangazwa kuwa mchezaji mpya wa Man United.

Taarifa zaidi zinaeleza kiungo huyo aliondoka kwenye kambi ya timu ya taifa baada ya kumalizika kwa mchezo wa kirafiki kati ya Brazil na Croatia kwa ajili ya kwenda kufanyiwa vipimo.

Dau la usajili la kiungo linatajwa ni kiasi cha pauni milioni 52. Kwa sasa kiungo huyo yuko nchini England, akiwa na timu yake ya taifa ya Brazil.

Fred alijunga na klabu ya Shaktar mwaka 2013 na alikuwa ni sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kilichoshiriki michuano ya Copa America 2015.