Diamond Amtolea Mapovu Dada yake Esma

Bado drama zinaendela mara baada ya Diamond kuachia video ya wimbo ‘Iyena’ ambao katika video yake anaonekana aliyekuwa mpenzi wake, Zari The Boss Lady.

Time hii ni kati ya Diamond na dada yake, Esma Platnumz ambapo Diamond amejibu kile alichozungumza Esma hapo jana.

Kama unakumbuka jana Esma alieleza kuwa amemmisi Zari ambaye alimtaja kama wifi yake wa kimataifa na kueleza kuwa umuhimu wa mtu anaona pale anapokuwa hayupo.

Alienda mbali zaidi kwa kueleza kutokana na hilo kuna mtu (Diamond) ana msongo wa mawazo na amekonda, pia kwenye moja ya interview alisema hilo pia. Sasa Diamond amejibu kupitia ukurasa wake wa Instagram;


Unajua bado nakutafakari, Hivi dada yangu ile interview yako ya jana, ni Swaumu ilikuwa kali ukaamua umalizie Hasira zako kwangu ama???.

Maana kusema pengine ulilewa kwa mwezi huu mtukufu Hapana. Yaani jana, kama sio wewe vile uliyekujaga na Hamisa kwenye Birthday na 40 ya Nillan na sare Mkashona, na kutunza juu….Dah Mungu anakuona.

Kumbuka drama zote hizi zinaletwa na wimbo ‘Iyena’ ambao ulitoka hapo jana June 01, 2018 na kuweza kufikisha views milioni moja katika mtandao wa Youtube ndani ya saa 19 pekee.