Davido kusherehekea sikukuu ya Eid na Watanzania

Hit maker wa IF, Fall , FIA na nyingine nyingi, David Adedeji Adeleke aka Davido anatarajia kufanya show ya nguvu siku ya Sikukuu ya Eid mbele ya wakazi wa Dar es salaam kwa mujibu wa bosi wa King Solomon, Solomon Nasuma.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo, Assurance amekuwa ni mmoja kati ya wasanii wanaofanya vizuri zaidi kwa Afrika baada ya kutajwa katika kinyang’anyiro cha tuzo za BET katika kipengele cha ‘International Act’ akiwa na wakali wengine wa Afrika kama Cassper Nyovest wa South Africa, Fally Ipupa wa DRC, Tiwa Savage wa Nigeria pamoja na Kundi la Distruction Boyz kutoka Afrika Kusini.

Akiongea na wadau waliojitokeza katika uzinduzi wa wimbo ‘Sheba’ ya Kundi la The Mafik uliofanyika Club Next Door wiki hii, bosi huyo aliwataka watu waliohudhuria ukumbini hapo kukaa mkao wa kula kwaajili ya show kubwa ya Davido katikati ya mwezi huu.

Bosi huyo hakuweka wazi kama show hiyo itafanyikia katika ukumbi wa Club Next Door Masaki au katika ukumbi mkubwa ya King Solomon Hall uliopo Namanga jijini Dar es salaam.

Watanzania kwa sasa wanaisubiria kwa hamu show hiyo ya aina yake kutokana na muimbaji huyo kufanya vizuri katika show zake ambazo amekuwa akizifanya nchi mbalimbali kupitia ziara yake ya muziki ya The 30 billion African Tour.


Muimbaji huyo amekuwa na mafanikio makumbwa mwaka 2017/18 baada ya ngoma zake mbili kwa pamoja kufanya vizuri duniani, ambapo ngoma ya ‘IF’ ikifikisha mauzo ya Diamond huku ‘Fall’ ikifikisha mauzo ya Platnumz.