Binti wa Kiganda Aeleza Sababu za Kujiteka


Nakusogezea hii kuhusu Jeshi la Polisi ambapo limemkamata mtoto wa miaka 15 baada ya kufeki kutekwa na kubakwa ili ajipatie fedha kwa baba yake nchini Uganda.

Msichana huyo alimpigia simu baba yake David Kazibwe, akimwambia kuwa ametekwa na wanaume wanne ambao wanahitaji Shilingi Milioni 30 za kiganda ambazo ni sawa na zaidi ya Milioni 18 za kitanzania ili aachiwe huru jumamosi iliyopita.

Afisa wa kituo cha polisi cha Bujuuko Emmy Nuwagira amesema kuwa Kazibwe aliwaarifu polisi baada ya mtoto wake huyo kurudi nyumbani na baada ya kumuuliza alikuwa wapi alidai kuwa amefanikiwa kuwatoroka watekaji.

Kazibwe aliwaambia polisi pia baada ya kurudi nyumbani alikuwa akilalamika kuwa anasikia maumivu makali  yaliyosababishwa na kubakwa na kundi hilo la wabakaji.

Baada ya kumpeleka kituo cha polisi kwa ajili ya kuandika maelezo na punde polisi kuanza kumhoji waligundua kuwa maelezo yake yanakinzana na ndipo walipoamua kumpeleka katika kituo cha afya cha Nyange ili akafanyiwe vipimo.

Kwa mujibu wa ripoti ya daktari ni kuwa mtoto huyo ni bikira yaani hajawahi kufanya tendo la ndoa katika maisha yake yote  na wala  hakuwa na majeraha yoyote kwenye mwili wake.

Hata hivyo mtoto huyo alikubali baadae mwenyewe kuwa alifeki kutekwa ili apate fedha kutoka kwa baba yake ili aanzishe biashara yake.

“Nilikuwa nimechoka kukaa nyumbani hivyo nilikuwa nataka baba anipe hela nikaanzishe maisha yangu mapya sehemu nyingine” alisema mtoto huyo.

Kwa sasa mtoto huyo anashikiliwa katika kituo cha polisi cha Bujuuko kwa kutoa taarifa za uongo na kufeki kutekwa. 
MaoniMaoni Yako