Friday, June 8, 2018

Bavicha: Kuzuia mikutano ya siasa kumeua vipaji vya uongozi

 Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Patrick ole Sosopi amesema hatua ya Serikali kupiga marufuku shughuli za kisiasa imeua vipaji vya vijana wengi wanaotegemea kuwa viongozi.


Ole Sosopi amesema hayo leo Ijumaa Juni 8 katika mahojiano maalumu alipotembelea ofisi za Mwananchi jijini Dar es Salaam.


Amesema hatua hiyo imesababisha wanasiasa kufanya kazi katika mazingira magumu lakini kamwe hawatanyamaza, wataendelea kuipinga hatua hiyo.


“Jambo hili haliathiri Chadema pekee, linawaathiri watanzania wengi. Ila sema sisi ni champion wa kulipigania, kulipigia kelele ili kuhakikisha tunapata mazingira bora ya kufanya siasa na kunakuwapo uhuru wa kujieleza,” amesema.


Amesema miongoni mwa athari za kuzuia shughuli za kisiasa ni vijana kupoteza vipaji vya kisiasa, kwa kuwa yanakosekana mazingira ya kuwaibua wenye uwezo wa uongozi kama walivyokuwa wanapatikana kwenye mikutano ya hadhara na makongamano.


“Ni lazima tupige kelele, Rais Magufuli yeye umri unaenda, lakini wapo vijana ambao tunatarajia waonyeshe vipaji vyao, ndio maana tumekuwa tukiwafuata kwenye mafunzo, mahafali na mikusanyiko ili kuona kina nani wenye uwezo,” alisema.


Amsema kutokana na hatua hiyo mtu ambaye anafikiri leo kuwa mwenyekiti wa kijiji, diwani au mbunge hana nafasi ya kuonyesha uwezo wake kama ilivyokuwa hapo awali.Sosopi ambaye pia ni mjumbe wa kamati Kuu ya Chadema amesema kutokana na hatua hiyo wananchi wengi wamejenga chuki ambayo inavinufaisha vyama vya upinzani na hivyo kujiongezea wafuasi.

No comments:
Write comments

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();

Facebook