Banka amshauri Niyonzima

ALIYEKUWA winga wa Simba, Mohamed Banka amesema kiwango alichokionyesha Haruna Niyonzima akiwa Yanga, hakustahili kuendelea kucheza timu za Tanzania badala yake angeangalia madili ya nje.
Anakiri kwamba Niyonzima ana uwezo wa hali ya juu na kwamba angeacha kucheza lgi kuu ya VPL kwa kulinda  heshima ya kiwango chake, kuliko akasubiri uwezo uishe ndipo aondoke.
"Siwezi kumjaji Niyonzima kushindwa kucheza msimu huu, najua majeruhi ndio yamemnyima raha, ila kwa uwezo wake asikubali aishushe heshima yake kwa kuhama hama timu.
"Mfano mzuri ni wale wachezaji wa Azam FC, Pascal Wawa na Kipre Tcheche wameondoka nchini wakiwa na uwezo wa hali ya juu na ndio maana wanakumbukwa mpaka sasa, lakini kama uwezo wao ungekuwa chini thamani yao isingekuwepo,"anasema.