Baba Mwenye Nyumba Asiyedai Kodi, Anayewahudumia Wapangaji huko Uganda

Katika Instagram ya Millardayo jana alikuwekea short story ya Baba mwenye nyumba asiyedai kodi na anawahudumia wapangaji wake sasa leo May 31, 2018  nakusogezea full story juu ya Baba mwenye nyumba mmoja nchini Uganda anayeitwa Kenneth Mubiru amewashangaza wengi jinsi ambavyo anaishi na wapangaji wake.

Mpangaji mmoja wa Mubiru anasimulia kuwa bwana huyo hajawahi kuwafuata akidai kodi ya nyumba bali wao wapangaji ndio huwa wanampigia simu na kumuomba aende akachukue fedha hizo.

“Na ukimpigia simu anaweza kuja kuchukua fedha hizo mwezi unaofata na tena mpaka umtishie kwamba utazitumia fedha na cha ajabu atakwambia tumia kidogo tu unayoweza kurudisha” alisema mpangaji huyo.

Anaendelea kusimulia kuwa kuna kipindi aliwahi kukaa miezi mitatu hajalipa kodi na alitegemea Mubiru kumpigia simu akimdai kodi lakini mambo yalikuwa tofauti. Mubiru alinisubiria mpaka nilipopata fedha ndipo nikalipa na alinishukuru sana badala ya kunilalamikia kuwa nimechelewesha kodi.

Mpangaji huyo anasema kuwa baba mwenye nyumba ana mashamba hivyo huwaletea mazao kila mpangaji wake bure kabisa na kama kuna kitu kimeharibika kwenye nyumba basi atakirekebisha bila kulalamika.

Aidha Mubiru akijua mpangaji wake anaumwa basi atakuwa anamjulia hali yake kila siku na atakuwa akimpelekea chakula mpaka atakapojisikia vizuri.

Hata hivyo Mubiru hapendi mambo yasiyokuwa na maadili katika nyumba yake ijapokuwa hajawapangia sheria za namna ya kuishi katika nyumba yake.

Unaambiwa hivi wapangaji huondoka kwenye nyumba ya bwana Mubiru wakiwa wanahamia kwenye nyumba zao na si vinginevyo. 
MaoniMaoni Yako