Saturday, June 2, 2018

Amber Lulu, Ngoma Ikivuma Sana Ujue Inakaribia Kupasuka

Tags


UPO usemi wa wa­henga kwamba ngoma ikivuma sana, basi ujue inakaribia kupasuka! Msemo huu unaweza kuwa un­ashabihiana sana na maisha anay­oishi mwanadada Amber Lulu.

 Juzikati amefanya kitendo kinachochefua mno, hasa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan. Amber Lulu akiwa na msanii mwenzake, Nuh Mziwanda, wamejirekodi video wakifanya uchafu ambao hauandikiki gazeti, kwa walioiona video hiyo iliyoza­gaa kwenye mitandao ya kijamii watakuwa wananielewa.

Nimebahatika kumsikia Nuh Mzi­wanda akijitetea kwamba alikuwa ‘location’ kurekodi video ya wimbo wake mpya, ndipo Amber Lulu ‘al­ipomlazimisha’ kurekodi video hiyo, utetezi wa kitoto kabisa! Nitakuja kuzungumza na Nuh Mziwanda siku nyingine lakini leo nataka kum­zungumzia Amber Lulu.

 Katika utetezi wake wakati akizungumza na Global TV Online, Amber Lulu anasema kwamba walikuwa kurekodi kazi yao mpya waliyoshirikishana na kwamba hakuna chochote kibaya alichoki­fanya bali alikuwa ‘akimkisi’ Nuh Mziwanda, sehemu ambazo wengi hawajazoea.

Kuhusu nani aliyesambaza video hiyo, Amber Lulu anajibu kirahisi ka­bisa kwamba mambo ya ‘snapchat’ ndiyo yamesababisha kwa sababu yeye alizisevu kwenye simu yake ikiwa haina ‘bando’ lakini baadaye ‘zikajiposti’. Majibu yake pekee yanatosha kuonesha Amber Lulu ni mtu wa namna gani.

 Kwa wasiomfahamu, mwa­nadada huyu alianza kama video queen, akiuza nyago kwenye video mbalimbali za wasanii wa Bongo.

Ni katika kipindi hichohicho akiwa hata bado hafahamiki vizuri, alianza drama za kukaa nusu utupu kwenye video alizokuwa akishirik­ishwa au kwenye picha alizokuwa akipiga na kuzitupia mitandaoni.

Ghafla umaarufu wake ukawa mkubwa, kila mtu akawa anatamani kumjua msichana huyo anayetisha kwa kukaa nusu utupu ni nani? Kama ni kiki ya kutokea, kweli alifanikiwa kuipata, tena sana tu! Jina lake likaanza kuwa maarufu kila mahali.

 Siku ziliendelea kusonga mbele, drama za Amber Lulu nazo zikawa zinazidi kuongezeka, baadaye akajiongeza kutoka kwenye u-video queen na kuhamia kwenye Bongo Fleva, nampongeza kwa hilo.

Skendo zake hazikuishia kwenye kupiga picha za kihasarahasara tu, bali pia zilihamia kwenye mapenzi. Tetesi za hapa za pale zikaanza ku­zagaa kwamba anaibanjua amri ya sita na msanii David Genzi ‘Young Dee’. Sakata lao lilienda mbali zaidi mpaka Young Dee akaingia kwenye matatizo makubwa na mama wa mtoto wake.

 Katika kipindi hicho akiwa anach­angia shuka na Young Dee, zikavuja picha kwenye mitandao ya kijamii na kuzua gumzo kubwa. Amber Lulu na Young Dee walipiga picha, msichana huyo akiwa amejistiri kwa kufuli tu, huku Young Dee akiwa kifua wazi, tena katika mkao usiofaa kuonekana hadharani.

Baadaye Young Dee alimtuhumu Amber Lulu kwamba ndiye aliyevujisha picha hizo! Hilo likapita, zikafuata drama nyingi tu za mwa­nadada huyo mpaka mwisho alipo­jikuta kwenye mikono ya serikali.

 Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza akamtaja kama mion­goni mwa wasanii wenye tabia ya kupiga picha za utupu na kuzianika mitandaoni, akapewa onyo kali na kukabidhiwa kwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ili aendelee kuc­hunguzwa.

Ungeweza kudhani kwamba baa­da ya mwanadada huyo kuwekwa mtu kati na serikali, pengine anawe­za kubadilika lakini wapi! Ndiyo kwanza akawa ameongezwa kasi! Penzi lake na msanii Prezoo kutoka nchini Kenya, ni ushahidi kwamba Amber Lulu ameshindikana!

 Mara kwa mara wamekuwa wakipiga picha wakifanya mambo ambayo hayaandikiki, yanayotakiwa kufanywa chumbani kwa siri, lakini unashtukia Amber Lulu ameposti kwenye mitandao ya kijamii.

Unajaribu kujiuliza, kama hiki ndiyo kizazi cha wasanii tulionao, ambao hawawezi ku-survive mjini bila kutegemea kiki, tena wakati mwingine kiki ambazo si tu zinadhalilisha utu wao, bali zi­naenda kinyume kabisa na maadili, tunaandaa kizazi gani?

 Watoto wa kike ambao leo wapo shuleni, wakimtazama Amber Lulu na kuamini kuwa kile anachokifan­ya ndicho anachotakiwa kukifanya msanii wa kike, miaka michache baadaye tutakuwa na kizazi cha aina gani?

Upuuzi alioufanya na Nuh Mzi­wanda, ni mwendelezo tu wa tabia za hovyohovyo alizonazo Amber Lulu. Lazima ifike ma­hali, Amber Lulu ubadilike.

 Yawezekana uchakaramu ni asili yako, lakini kwani hauwezi kuwa na staha japo kidogo, hasa katika zama hizi ambazo intaneti inasam­baza taarifa kwa kasi kubwa na zitaendelea kuwepo huko mpaka utakapozeeka?

Unataka kesho na kes­hokutwa ukiwa na watoto wajifunze nini kutoka kwako? Unataka jamii ikutafsiri katika kundi gani? Njaa zisikufanye ukaud­halilisha utu wako, take care!