Powered by Blogger.

Slider

Breaking

KITAIFA

VideoBar

This content is not yet available over encrypted connections.

KIMATAIFA

MAGAZETI

UDAKU

BURUDANI

SPOTI TV

» » Zama Za Yaya Toure Zimefikia Ukingoni Etihad , Guadiola Asema haya.. Kwaheri Toure

Mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast na Manchester City, Yaya Toure hatimaye anaondoka City baada ya kuitumikia Klabu hiyo kwa jumla ya Mechi 229 kwa kipindi cha zaidi ya miaka nane 8. Toure atacheza katika mchezo wa City dhidi ya Brighton katika ligi ya EPL, Pep Guadiola aliliambia SPOTI TZ.

Mchezaji huyo kipenzi na mtaalamu wa kandanda pale katikati ya uwanja ametoa mchango wake kiasi kidogo katika msimu huu, akiwa na miaka 34 mkataba wake utaisha mwishoni mwa msimu huu wa 2017/2018
“Yaya hatakuwa nasi hapa City msimu ujao” Guadiola alimwambia Mwandishi wetu, Guadiola alisema hayo wakati mabingwa hao wa EPL wakijiandaa na mchezo wao dhidi ya Brighton utakaopigwa siku ya Juma Pili. Na Yaya anatarajiwa kuwepo ndani ya dimba kama mchezo wake wa mwisho na kuaga mashabiki wake wa Etihad
“Mchezo wetu na Brighton tutautumia kumpa heshima anayostahili, moja kati ya njia nzuri na ya heshima kabisa mchezaji anaweza kupewa kama namna ya kumuaga, tutakuwa tunadhamira ya kushinda kwaajili ya Yaya na tutashinda kwaajili yake” aliongeza Mhispaniola huyo.
Toure alijiunga na City akitokea Barcelona, kipindi ambacho Guadiola alikuwa anafundisha Barcelona kama Kocha mwaka 2010. Na sehemu ya msimu uliopita alikosa michezo mingi baada ya kutokea kurushiana maneno kwa Wakala wa Toure na Kocha wake huyo, Mhispaniola Guadiola.
Mchezaji huyo atakayefikisha umri wa miaka 35 mwezi huu, baadaye aliomba msamaha kwa kocha wake kutokana na kitendo cha Wakala wake kutoleana maneno katika vyombo vya habari na Kocha wake huyo. Msamaha huo ulimfanya Toure aongezewe mkataba wa mwaka mmoja.
Amecheza michezo 229 katika ligi ya EPL, kwa kipindi cha miaka 8 nane, lakini amecheza michezo tisa 9 tu katika msimu huu. Amefanikiwa kushinda mataji mawili, FA na mawili ya EPL.


«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post