Yondani apotea kusikojulikana, Uongozi watoa tamko


Na George Mganga

Wakati Yanga ikianza maandalizi ya kujiandaa na safari ya kesho kuelekea Kenya kwa ajili ya michuano ya SportPesa Super Cup, taarifa zinaeleza kuwa beki wake, Kelvin Yondani, ametimkia kusikojulikana.

Yondani hajacheza mchezo wowote tangu agungiwe na Bodi ya Ligi ya TFF baada ya kumtemea mchezaji wa Simba, Asante Kwasi katika mchezo uliowakutanisha watani hao wa jadi, Simba na Yanga, Aprili 29 2018 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa amelitolea ufafanuzi kuhusiana na kutopatikana kwa Yondani akieleza kuwa amepatwa na matatizo ya kifamilia hivyo atarejea kikosini siku yoyote.

Akizungumza na Radio EFM, Mkwasa amesema suala la mchezaji kutokuwa hewani kupitia simu yake haina maana ya kwamba hawezi kuonekana na akieleza kuwa ni jambo la kawaida pekee.

Mbali na hilo, Mkwasa amesema Yondani bado ni mchezaji wa wao kwa kuwa bado ana mktaba na Yanga licha ya kuwepo kwa tetesi kuwa Simba wanamuwinda kwa ajili ya kumsajili.

Yondani alifunguliwa kifungo chake kalba ya mechi dhidi ya Azam kufuatia kitendo chake cha kumtemea mate Kwasi katika mchezo dhidi ya Simba ambao Yanga walikubali kichapo cha bao 1-0.

MaoniMaoni Yako