Yondani ajulikana alipo baada ya kupotea


Beki wa Yanga aliyeripotiwa kupotelea kusikojulikana, Kelvin Yondani, ameonekana leo katika makao makuu ya klabu hiyo akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika.

Yondani ambaye alikuwa hapatikani kupitia simu zake za mkononi aliripotiwa kutokomea kusikojulikana huku akishindwa kuwa na kikosi cha Yanga tangu mchezo dhidi ya Simba uliopigwa Mei 29 2018.

Baada ya kuwasili kunako makao makuu ya klabu leo, taarifa zimeelezwa kuwa amefanya mazungumzo na Yanga ili kuweza kuongeza mkataba mwingine.

Ikumbukwe mkataba wa Yondani na Yanga unamalizika mwaka huu hivyo Nyika amefanya mazungumzo na beki huyo kuweza kuongeza ili aendelee kuitumikia klabu
MaoniMaoni Yako