Sunday, May 27, 2018

Yaya Toure kuibukia katika Uchambuzi Kombe la Dunia wakati Kiswahili Kikipewa Chapuo

Tags

Katika michuano ya Kombe la Dunia mwezi ujao June 14 kutakuwa na wachambuzi  maarufu wa Soka ambao wengi wetu tungetamani kuwaona kupitia  katika kituo cha Super sport

Yaya Toure, miongoni mwa magwiji wa Mpira wanaopendwa sana barani Afrika na Duniani kote atakuwa katika meza hiyo ya mduara kuchambua michuano hiyo. Toure ataungana na Jay – Jay Okocha, Dwight Yorke pamoja na Beki wa zamani wa Manchester United Phil Neville na Muitaliano Maestro- Gianfranco Zola mmoja kati ya wachezaji mashuhuri kabisa wa Chelsea nyakati hizo.

Super sport watakuwa hewani kwa masaa 24 kupitia chanel  ambayo tayari ipo hewani maalumu kabisa kwaajili ya Kombe la Dunia. (ss3) Lugha zitakazotumika ni Kiswahili, Kiingereza , Kireno Kizulu na Kisotho