Yanga yawaonya simba juu ya suala la kuvizia wachezaji wake


Baada ya kuelezwa kwa baadhi ya wachezaji Yanga kuwa wanaondoka ndani ya klabu hiyo kutimkia mahala pengine, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika ameeleza kuwa hawawezi kuruhusu mchezaji mwingine aondoke zaidi ya Ngoma.

Nyika amepiga mkwara huo kutokana na taarifa mbalimbali kuripotiwa kuwa wachezaji wao wengi wanaweza kuondoka ikiwa dirisha la usajili linatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni.

Kiongozi huyo ameeleza kuwa bado wachezaji wote wapo pamoja na Yanga, na endapo ikitokea wakaondoka labda uongozi wenyewe uamue wafanya hivyo.

Ikumbukwe mpaka sasa Yanga imesharuhusu Ngoma kutimkia Azam FC huku baadhi ya wachezaji wake wengine wakielezwa kutaka kuihama timu hiyo.

Papy Tshishimbi, Kelvin Yondani, Andrew Vincent na Juma Abdul ni miongoni mwa wachezaji walio katika tetesi zinazohusishwa kutimkia Simba au Azam FC.

MaoniMaoni Yako