Yanga yatua Dubai


Dubai. Yanga wamewasili Dubai ambapo kesho saa 2.45 asubuhi wataunganisha ndege kwenda Algeria.
Msafara wa Yanga ukiongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Salum Mkemi uliwasili Dubai mnamo saa 4.52 usiku kwa saa za huku na kufanyiwa ukaguzi kabla ya kwenda katika eneo maalum la abiria wanaounganisha ndege kupumzika.
Mbali na Mkemi, kiongozi mwingine aliyeambatana na kikosi cha Yanga ni Mwenyekiti wa Kamati za Mashindano na Usajili, Hussein Nyika ambaye amekuwa akisafiri na timu hiyo mara kwa mara.
Maofisa wa benchi la ufundi ni Meneja Hafidh Saleh, Kocha Mkuu Mwinyi Zahera, makocha wasaidizi Shadrack Nsajigwa na Noel Mwandila, daktari Edward Bavu na Mtunza Vifaa, Mahmoud Omary 'Mpogolo'.
Pia mchua misuli, Jackob Onyango ni sehemu ya maofisa wa benchi la ufundi ambao wameambatana na timu
Chanzo: Mwanaspoti
MaoniMaoni Yako