YANGA YAPIGWA MARA 4 KATIKA LIGI BAADA YA KUFUNGWA NA MTIBWA LEO


Hali imezidi kuwa ngumu kwa Yanga katika ligi msimu huu baada ya kukubali kupoteza tena mchezo wa leo dhidi ya Mtibwa Sugar kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Kikosi hicho kimeondoka na alama sifuri baada ya kutoka kufungwa na Tanzania Prisons kwa mabao 2-0 katika mchezo uliopita kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya

Bao pekee la mchezo huo limefungwa na Hassan Dilunga katika dakika ya 82 ya kipindi cha pili na kuufanya mchezo umalizike kwa matokeo hayo.

Yanga imepoteza jumla ya michezo minne sasa katika Ligi baada ya kufungwa na Mbao katika mzunguko wa kwanza wa ligi, kisha Simba, baadaye na Tanzania Prisons na leo dhidi ya Mtibwa Sugar.

Matokeo haya yanaifanya Yanga kuendelea kusalia nafasi ya tatu kwa kuendelea kuwa na alama zake 48.

Ushindi huo kwa Mtibwa umeiongezea pointi tatu muhimu kwa kufikisha 37 ikiwa nafasi yake ya 6.
Credit: Saleh Jembe