YANGA yakutana tena dar kuandaa kipigo cha rayon sportsNa George Mganga

Baada ya kugawanyika kimafungu kwa muda, kikosi cha Yanga kimeungana kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rayon Sports.

Yanga wameungana baada ya kutengana kwa muda ambapo baadhi ya wachezaji walikuwa nje ya Dar es Salaam kwa ajili ya mechi za ligi na wengine wakisalia Dar kujiandaa na mchezo huo wa kimataifa.

Tayari wachezaji wote wapo kambini hivi sasa kujiandaa na vita dhidi ya Rayon, mechi itakayopigwa Mei 16 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Yanga inaingia kucheza kibarua ikiwa na kumbukumbu mbaya za kupoteza mchezo uliopita dhidi ya USM Alger kwa kuchapwa bao 4-0.

Mchezo umepangwa kufanyika saa moja za usiku ili kuwapa nafasi mashabiki watakaokuwa kazini kuwahi mechi hiyo.

Source: Saleh Jembe

MaoniMaoni Yako