Yanga Yaawakataa Wacongo 2 Wa Zahera.


Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu ya Yanga, Hussein Nyika amewakataa wachezaji wawili kutoka DRC Congo, mshambuliaji Alain Mulumba aliyetoka Motema Pembe, na Kiungo Cedrick Kabale aliyetoka Don Bosco.

-Mwenyekiti huyo alikuwa anahudhuria mazoezi ya Yanga kila siku kuanzia siku ya Alhamisi kuangalia mazoezi ya timu na wachezaji hao wawili walianza majaribio na mshambuliaji kutoka Nigeria, James Ogochukwu.


-Hussein Nyika akagudua waCongo hao ni weupe tena wakawaida muno baadae akaongea na bechi la ufundi la klabu hiyo ambalo liko chini ya Mwandila kwa sasa akaambiwa tena wale wacongo ni wakawaida muno bora yule mshambuliaji kutoka Nigeria anaonekana anaweza akapambana.

-Baada ya Mwenyekiti huyo kujua wale waCongo ni weupe amesitisha mpango wa klabu hiyo kusajili wachezaji wa kimataifa kwa kuja kufanya majaribio sasa watakuwa wanasafirisha kocha kwenda kumuona mchezaji yoyote kwenye timu yake kabla ya kumsajili. Kama walivyoweza kuwasajili Papy Tshishimbi, Donald Ngoma na Thaban Kamusoko.

-Wachezaji hao walikuwa wanafanya majaribio kwenye klabu hiyo ila walikuwa wanamsubili kocha mkuu wa klabu hiyo Mwinyi Zahera ambaye yupo Kwao Congo kuja kutoa maamuzi ya mwisho kuhusu usajili wa wachezaji hao.

-Yanga ina mpango wa kusajili wachezaji watatu wa kimataifa ili kuwatumia kwenye kombe la shirikisho. Yanga tayari wameachana wachezaji wao 2 wa kimataifa Donald Ngoma ambaye ameelekea Azam na Festo Kayembe aliyetimukia kwao Congo pia Yanga wana mpango wa kumtema golikipa wa kikosi hicho Youthe Rostand na kumsajili Ley Matampi wa Tp Mazembe.

MaoniMaoni Yako