Yanga wanapiga tizi la mwisho leo kwa kazi maalum ya kuwamaliza mtibwa kesho huko morogoro


Kikosi cha Yanga kinafanya mazoezi ya mwisho mjini Morogoro leo tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar.

Yanga itakuwa mgeni katika mchezo huo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini humo kesho Mei 13 2018.

Kikosi hicho kinaenda kupambana na Mtibwa kikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Tanzania Prisons kwa kufungwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mechi hiyo itakuwa ni ya kukamilisha ratiba kwa timu zote mbili baada ya Simba kutangazwa kuwa mabingwa kutokana na kufikisha alama 65 ambazo hazitafikiwa na timu klabu nyingine yoyote.

Baada ya mchezo huo kikosi kitarejea jijini Dar es Salaam kuendelea na mazoezi ya kujiandaa na mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda.

Kuelekea mechi hiyo ya kimataifa, Nahodha wa Yanga, Kelvin Yondani, ameanza mazoezi baada ya kupona majeraha yake na inawezekana akawa sehemu ya mchezo dhidi ya Rayon Mei 16 2018 kwenye Uwanja wa Taifa.
Credit: Saleh Jembe
MaoniMaoni Yako