YANGA: Simba ilituharibia mbio za ubingwaKufuatia kufanya vibaya katika mechi za ligi, baadhi ya mashabiki wa Yanga wamesema kuwa Simba ndiyo iliwapotezea mwelekeo wa kutetea ubingwa wao.

Yanga imepoteza mechi tatu mfululizo hivi sasa ikiwa ni dhidi ya Simba, Tanzania Prisons na Mtibwa Sugar FC.

Mashabiki hao wameeleza kuwa kitendo cha kupoteza dhidi ya Simba Aprili 29 2018 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, uliwakata maini wachezaji wa kikosi hicho kwa kuondoa hali ya kujiamini kwenye michezo iliyofuatia.

Baadhi yao wanaamini kama wangepata matokeo kwenye mechi na Simba, wangeweza kupata nguvu na morali ya kujituma zaidi kuendelea kuutetea ubingwa wao waliouchukua mara tatu mfululizo.

Yanga juzi imekubali kipigo kingine dhidi ya Mtibwa Sugar kwa kufungwa bao 1-0 na kuendelea kusalia katika nafasi yake ya 3 ikiwa na pointi 48.

Source: Saleh Jembe

MaoniMaoni Yako