Yanga mechi 7 bila ushindi inakwama wapi?

Yanga imecheza mechi saba bila ushindi katika mashindano yote inayoshiriki (ligi kuu Tanzania bara na Caf Confederation Cup).

Mechi sita ambazo Yanga haija ni Wolaitta Dicha 1-0 Yanga, Mbeya City 1-1 Yanga, Yanga 1-1 Singida, Simba 1-0 Yanga, USM Alger 4-0 Yanga, Tanzania Prisons 2-0 Yanga na Mtibwa Sugar 1-0 Yanga.

Leo Jumapili Mei 13, 2018 Yanga ilikuwa ugenini ikicheza na Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo wamepoteza mchezo huo kwa kufugwa goli 1-0.

Baada ya kufungwa 2-0 na Tanzania Prisons kwenye mechi iliyopita, Yanga imepoteza mchezo wa pili mfululizo kufuatia kipigo cha leo.

Hadi sasa Yanga imepoteza mechi nne za ligi baada ya kucheza mechi 26 huku ikiwa na mechi mbili mkononi (viporo). Mechi zote ambazo Yanga imepoteza ilicheza ugenini (Mbao 2-0 Yanga, Simba 1-0 Yanga, Tanzania Prisons 2-0, Mtibwa Sugar 1-0 Yanga).

Imepoteza mechi tatu mfululizo kati ya nne, Simba 1-0 Yanga, Tanzania Prisons 2-0 Yanga, Mtibwa Sugar 1-0 Yanga. Katika mechi hizo, Yanga haijafanikiwa kufunga goli hata moja.

Yanga inaendelea kubaki nafasi ya tatu kwenye  msimamo wa ligi ikiwa na poini 48 nyuma ya Azam (pointi 52) na Simba (pointi 68). Ushindi dhidi ya Yanga unaifanya Mtibwa Sugar ifikishe pointi 37 na kukaa katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi.

Source: Shaffih Dauda

MaoniMaoni Yako