Yanga anatoka mzimbabwe anaingia mzimbabwe

Yanga wapo katika Kipindi cha Kuhakikisha wanafumua Kikosi chao na Kukifanya kuwa na Makali ya Kutosha kwaajili ya Mashindano yote Yajayo ndani Na Nje ya Nchi.

Baada ya Kuthibitika kuwa Yanga imeachana na Mshambuliaji wake Nyota Mzimbabwe Donald Ngoma Kuna Mzimbabwe Mwingine Anatua Yanga.

Mzimbabwe Huyo  ni Tafadzw Kutinyu ambaye anacheza Singida United, Taarifa za Kuaminika ambazo tumezipata Ni kwamba Kutinyu anaasilimia Kubwa Kutua Yanga licha ya Kutajwa pia Azam Fc.

Kuna Taarifa kuwa Kutinyu anashawishiwa kwenda Azam kwa Kocha Hans Van Pluijm lakini Inadaiwa kuwa Kutinyu anavutiwa zaidi kucheza Yanga kuliko Azam na Kuna Kigogo wa Singida United anatajwa huenda akawasaidia Zaidi Yanga kumpata Kutinyu.

MaoniMaoni Yako