Powered by Blogger.

Slider

Breaking

MICHEZO

HABARI

MAGAZETI

UDAKU

BURUDANI

VIDEOS

» » Wanaoweza kumrithi Rostand Jangwani


KAZI iliyowashinda kina Deogratius Munishi ‘Dida’ na Ally Mustafa ‘Barthez’ pale Yanga inaelekea pia kumshinda Mkameruni, Youthe Rostand.
Ni kweli Yanga ni kati ya timu zilizoruhusu mabao machache katika Ligi Kuu Bara mpaka sasa ikiwa sambamba na Azam ikiruhusu mabao 14, ila yenyewe ina michezo pungufu. Yanga michezo yake ni 24 na Azam ina 27, lakini zimefungwa zaidi bao mioja iliyofungwa Simba iliyoruhusu 13 tu katika mechi 27.
Hata hivyo, kitendo cha kipa Rostand kufungwa kwa makosa ya aina moja inawachosha Wanayanga. Kipa huyo mrefu amekuwa akifungwa mipira ya krosi na kona na kumtia doa.
Rostand alijiunga na Yanga msimu huu akitokea African Lyon. Timu hiyo ilimsajili kwa lengo la kuwabeba kwenye mashindano ya kimataifa, lakini imekuwa vigumu kwa Rostand.
Mwenendo huo wa Rostand unaweza kumweka kwenye wakati mgumu msimu huu na huenda akasajiliwa kipa mpya.
Mwanaspoti linakuletea orodha ya makipa watano wazawa wanaoweza kuziba nafasi ya Mkameruni huyo kwa ufasaha.
AISHI MANULA
Kipa huyu wa Simba aliyesajiliwa akitokea Azam FC amecheza mechi zote katika ligi na kuwa chaguo la kwanza katika timu hiyo.
Katika mechi 27, ambazo Manula amecheza msimu huu amefungwa katika mechi nane na akiweza kuwazuia washambuliaji kutokugusa nyavu zake kutikiswa katika mechi 19.
Manula mwenye hadhi ya Tanzania One kwa sasa nchini, bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Simba lakini si jambo la kushangaza kusikia amekwenda Yanga kwani imeshawahi kutokea kwa makipa watatu wa Simba kwa nyakati tofauti kujiunga na Yanga ingawa kwa sasa inaweza kuwa vigumu kwa Yanga kumchukua kwa kutokana na hali ya ukata inayoikali timu hiyo yenye maskani yake Jangwani jijini Dare s Salaam.
Makipa waliowahi kuikacha Simba na kutua Jangwani ni pamoja na Juma Kaseja (sasa yuko Kagera Sugar), Barthez (sasa Singida United) na Dida (Afrika Kusini).
RAZACK ABALORA
Kipa wa Azam aliyesajiliwa msimu huu akitokea WAFA ya Ghana, naye anaweza kuziba nafasi ya Rostand vizuri. Abalora ameweza kuvaa viatu vya Manula pale Azam na kuwafanya mabosi wa timu hiyo kumsahau kabisa kipa huyo wa Simba.
Abalora amecheza mechi 21, huku akishindwa kucheza mechi sita baada ya kufungiwa mechi tatu, kisha benchi la ufundi la timu hiyo kuendelea na Mwadini Ally katika mechi zilizosalia.
Kiwango ambacho ameonesha Abalora anaweza kuwa miongoni mwa makipa wanaoweza kuziba nafasi ya Rostand ndani ya Yanga.
BENEDICTOR TINOCCO
Kipa wa Mtibwa Sugar, Tinocco amekuwa na msimu mzuri kwani katika mechi 26, ameruhusu mabao katika michezo 13 tu.
Tinocco amecheza mechi 21 msimu huu kwa kiwango cha juu huku nyingine tano akizikosa kwa sababu ya majeraha. Mechi hizo zilidakwa na kipa mkongwe, Shabaan Kado.
Japo kipa huyu aliwahi kuchemka aliposajiliwa Yanga kabla ya timu hiyo kumtoa kwa mkopo Mtibwa Sugar, anaweza kuwa chaguo sahihi kwa wakati huu kuziba nafasi ya Mkameruni huyo.
AGATHONY ANTHONY
Kipa huyu wa Lipuli katika mechi 27, amefungwa mabao 21 lakini ameonyesha kiwango cha kuvutia. Pamoja na kuruhusu mabao hayo, alicheza mechi tisa bila kuruhusu bao, hivyo kuwa miongoni mwa makipa wa viwango vya juu Ligi Kuu.
Kama atakuwa na kiwango hicho hadi mwishoni mwa msimu anaweza kutatajwa kwenda kuichukua nafasi ya Rostand pale Yanga kwani msimu huu amekuwa msaada katika kikosi cha Lipuli ambacho kipo nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi.
AARON KALAMBO
Kipa wa Tanzania Prisons ambayo ipo nafasi ya tano Ligi Kuu amekuwa akionesha uwezo wa kuokoa michomo mingi ya wazi na pengine asingekuwepo katika timu hiyo ingefungwa zaidi ya mabao 18, ambayo imeshafungwa mpaka sasa.
Kalambo ameruhusu mabao 18 katika mechi 18, ni wastani wa bao moja katika kila mchezo lakini kwa kiwango ambacho ameonesha mpaka sasa anaweza kuingia miongoni mwa mwa makipa ambao wanawania tuzo ya kipa bora wa Ligi Kuu.
Mbali na hilo Yanga inaweza kutuma maombi Prisons kumuhitaji kipa huyo ili kuziba nafasi ya Rostand kama ilivyofanya kwa Beno Kakolanya miaka miwili iliyopita.
Credit: Mwanaspoti

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post