Wachezaji wa Afrika waliomfaa Wenger huko Arsenal.Meneja wa Arsenal Arsene Wenger, amezungumza kuhusu kuwaenzi wachezaji kutoka Afrika wakati wa mkutano wake wa mwisho kama meneja ya klabu hiyo.
Kwenye mkutano wake wa mwisho na vyombo vya habari Wenger alisema wachezaji kutoka Afrika walikuwa wenye mchango mkubwa katika taaluma yake akiwa meneja wa soka nchini Uingereza.
"Tazama nilikuwa na wachezaji wa afrika maisha yangu yote. Nilifungua shule na moja wa marafiki zangu. Watu kama Yaya Toure, kama Kolo Toure kama Eboue, Gervinho walikuja nami kutoka shuleni," alisema Wenger.
"Nilkuwa na George Weah tangu akiwa na umri mdogo sana na Fofana kutoka Ivory Coast. Nilikuwa na Lauren kutoka Cameroon. Kawaida nilikuwa na wachezaji wa Afrika kwenye kikosi changu. Walikuwa wenye mchango mkubwa."
Wenger aliongoza mechi ya mwisho ya Arsenal jana Jumapili dhidi ya Huddersfield kwenye uwanja wa John Smith. Kikosi chake kiliibuka mshindi kwa bao 1-0.
Wenger anaondoka Arsenal baada ya kusimaima mechi 1,235 ambapo aliandikisha ushindi 716 na magoli 2,298. Arsenal bado hawajamteua mrithi wake.
Kuanzia Rais wa sasa wa Liberia George Weah huko Monaco hadi mchezaji wa mwisho aliyesaini raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, Wenger amekuwa mtu mihumu kwa wachezaji wa Afrika.
Kuwasaini na kuwakuza wachezaji bora zaidi wa Afrika ni kitu ambacho Wenger amekifanya katika miaka yake yote 22 amekuwa na Arsenal.
Sababu ya hili kutokuwa jambo la kushagaza, ni kuwa wachezaji 16 kutoka Afrika waliichezea Arsenal chini ya usimamizi wake Wenger.
Jeshi la Wenger kutoka Afrika:
 • Emmanuel Adebayor (Togo)
 • Alex Iwobi (Nigeria)
 • Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon)
 • Nwankwo Kanu (Nigeria)
 • Marouane Chamakh (Morocco)
 • Lauren (Cameroon)
 • Kaba Diawara (Guinea)
 • Quincy (Ghana)
 • Emmanuel Eboue (Ivory Coast)
 • Alex Song (Cameroon)
 • Mohamed Elneny (Misri)
 • Kolo Toure (Ivory Coast)
 • Emmanuel Frimpong (Ghana)
 • Armand Traore (Senegal)
 • Gervinho (Ivory Coast)
 • Christopher Wreh (Liberia)

Baadhi wa wachezaji
1. Nwankwo Kanu
Mshindi mara mbili wa tuzo la mchezaji bora Afrika, Nwankwo Kanu ni mmoja wachezaji bora zaidi kutoka Afrika kuwai kufanya kazi chini wa Arsene Wenger huko Arsenal.
Akiwa na Arsenal Mnigeria huyo alishinda vikombe viwili vya Premier League na FA na pia kombe la Community Shield.
Baada ya kujiunga na Arsenal mwaka 1999 Kanu alifunga magoli 44 kwenye mechi 198 alizocheza kabla ya kuhamia West Bromwich Albion mwaka 2004.
Anakumbukwa sana kwa hat-trick yake ya pili dhidi ya Chelsea.
2. Lauren
Raia wa Cameroon Lauren alifunga mabao 9 kwa mechi 241 alizocheza lakini kawaida alikuwa ni mchezaji aliyekuwa anategemegwa sana.
Alisainiwa na Wenger mwaka 2000 kama Wing'a na kuibuka kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi wa safu ya nyuma katika Premier League na hasa Arsenal hadi alipoondoka na kuelekea Portsmouth mwaka 2007.
Lauren alishinda vikombe vingi zaidi akiwa na Asenal chini ya Arsene Wenger.
3. Kolo Toure
Tumsahau mshambulizi Kolo Toure ambaye alikumbwa na matatizo nyakati za mwisho mwisho akiwa na Arsenal.
Sasa wacha tujikumbushe akisainiwa na Wenger kwa paunia 150,000, beki hiyo raia wa Ivory Coast ambaye pia alicheza kama mshambuliaji alikuwa mmoja wa wale waliotegemewa sana katika Premier League.
Toure alicheza na mawiji wengine kama Sol Campbell, William Gallas na pia Philip Senderos.
Alishinda mataji matano akiwa na Gunners na kuchangia mabao 14 kwa jumla ya mechi 326 alizocheza.
4. Alex Song
Alex Song alikuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi wa Afrika waliosainiwa na Wenger
Licha ya Song kutofikia kiwango cha watangulizi wake kama Patrick Viera na Gilberto Silva, alitoa mchango mkubwa kwa Arsenal.
Alikuwa ni mchezaji mzuri na hata badala ya kuhamia Portsmouth, aliamua kulekea huko Barcelona.
Hata hivyo hakushinda taji lolote akiwa na Arsenal.
Alisakata kambumbu ya hali ya juu kwenye mechi 218 akiwa na Wenger.
5. Emmanuel Adebayor
Yawezekana Emmanuel Adebayor alimuita Wenger mtu feki lakini bado anastahili kusmhukuru sana kwa kumkuza tangu alipomsaini kutoka Monaco mwaka 2006.
Adebayor haukuweza kuichezea Arsenal kwa misimu mitatu lakini ni mmoja wa wachezaji bora zaidi kuichezea Arsenal wakati wa kipindi cha Wenger.
Raia huyo wa Togo alicheza jumla ya mechi 143 na kufunga mabao 62.


source: bbc
MaoniMaoni Yako