Wachezaji majeruhi waiponza Simba

MABINGWA wa Ligi Kuu Bara Simba, msimu huu walikubali kichapo cha bao 1-0, kutoka kwa Kagera Sugar juzi Jumamosi katika siku ambayo walikabidhiwa kombe lao.
Kocha wa Simba, Mfaransa Pierre Lechantre alifunguka sababu moja wapo ya kupoteza mechi hiyo ambayo walikuwa wanataka kushinda ili kumaliza Ligi bila kupoteza mchezo wowote.
Lechantre alisema matokeo hayo ya kufunga yalimuumiza na alitaka kumaliza Ligi kwa kuweka rekodi ya kutokupoteza mechi yoyote katika msimu wake wa kwanza hapa akiwa Simba.
Anasema sababu moja wapo iliyochangia ni kutokuwepo fiti wachezaji wake wa kikosi cha kwanza ambao walikuwa majeruhi ilikuwa miongoni mwa sababu ya kupoteza ingawa mechi inamatokeo matatu.
“John Bocco, Nicholas Gyan, Juma Liuzio, Asante Kwasi na James Kotei licha ya wengine kuwalazimisha kucheza mechi bila ya kuwa fiti asilimia mia,” alisema Lechante ambaye alisisitiza kufanyia kazi makosa ambayo yalijitokeza kwenye mechi hiyo ili kushinda mechi ya mwisho na Majimaji.
Credit: Mwanaspoti
MaoniMaoni Yako