Wachezaji hawa wamefunika Simba Vs Yanga

 WIKIENDI iliyopita, Sim­ba iliendelea kuandika re­kodi katika Ligi Kuu Bara msimu huu baada ya ku­fanikiwa kuifunga Yanga bao 1-0 kwenye mchezo uli­opigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Ulikuwa ni mchezo am­bao uligusa hisia za wengi na kuwa na mambo mengi, lakini dakika 90 ndizo zili­weza kuamua mambo yote kwenye mchezo huo.

Lakini katika mchezo huo baadhi ya wachezaji wa Simba na Yanga waliweza kufanya vema kutokana na kuonyesha viwango bora, huku wengine wakipotezwa.

Baadhi yao licha ya kuwa na majina makubwa lakini walishindwa kuonyesha makali yao kwenye mchezo huo kama ambavyo imezoe­leka katika michezo mingine.
 Wafuatao ni baadhi ya wale ambao waliweza kuonyesha viwango bora kwenye mchezo huo.
JONAS MKUDE –SIMBA
Alikuwa ndiye mhimili mkuu kama siyo nguzo kwa upande wa Simba na aliweza kupam­bana na kutoa pasi ambazo zilifika vizuri kwa walengwa.
Mkude alipambana kwa kiasi kikubwa na kufanikiwa kuiendesha timu na kuisaidia kuondoka na pointi zote tatu. Katika nafasi ya kiungo wa kati, alimpiku Papy Tshishimbi wa Yanga.
 KELVIN YONDANI – YANGA
Licha ya timu yake kushindwa kupata matokeo mazuri, lakini uwezo wake wa kupambana kwa kiasi kikubwa uliweza kuonekana katika harakati za kuiokoa Yanga isipoteze mchezo.
Licha ya ubora wake nda­ni ya dakika tisini, Yondani hakufanya uungwana pale al­ipomtemea mate beki wa Sim­ba, Asante Kwasi.
 ERASTO NYONI – SIMBA
Ndiye aliyefanikiwa kuibeba zaidi Simba kutokana na bao lake alilolifunga dakika ya 38 kwa kichwa.
Bao la Nyoni katika mchezo huo limeendelea zaidi kuiweka Simba kwenye nafasi nzuri ya kuwania ubingwa msimu huu.
Nyoni alifunga bao hilo uki­wa ni mchezo wake wa pili wa ‘derby’ hiyo tangu ajiunge na Simba msimu huu akitokea Azam FC.
Katika mchezo huo al­ionekana kuwa bora kuto­kana na kiwango ambacho aliweza kukionyesha na uwezo wake wa kucheza nafasi zaidi ya moja anapokuwa uwanjani.
H A S S A N KESSY – YANGA
Licha ya kupewa kadi nyekundu baa­da ya kumchezea vibaya Asante Kwasi, lakini kwa muda aliocheza wa takriban dakika 48, alikuwa moto kwani aliweza kupam­bana vyema kwa kusaidia safu ya ulinzi.
Kessy kwa namna fulani ali­weza kuwadhibiti Emmanuel Okwi na Shiza Kichuya ili wasi­lete madhara katika lango lao.

SHIZA KICHUYA – SIM­BA
Mechi ya mzunguko wa kwanza ndiye aliyefunga bao kwa Simba katika sare ya 1-1. Safari hii ameshindwa kufunga lakini wikiendi iliyopita licha ya kutofunga, ndiye aliyetengen­eza bao lililofungwa na Erasto Nyoni na kuipa ushindi Simba wa bao 1-0.
Mara kadhaa Kichuya amekuwa msumbufu kwa wachezaji wa timu pinzani na ubora wake kila siku umekuwa ukionekana kuwa juu.
YOUTHE ROS­TAND – YANGA
Ni kipa wa Yanga na licha ya kufungwa bao kati­ka mchezo huo, lakini tunawe­za kumtaja kuwa ni mmoja wa mashujaa wa Yanga kutokana na kazi ya ziada aliyoweza kui­fanya ili timu yake isifungwe mabao mengi.
Haikuwa kazi rahisi kuwe­za kuokoa lakini alipambana na kuweza kuruhusu bao moja pekee na kama Yanga wangekuwa na kipa ambaye si imara basi huenda tunge­shuhudia mabao mengi zaidi.
ASANTE KWASI – SIM­BA
Sifa yake inajulikana ni beki pekee mwenye mabao mengi mpaka sasa katika Ligi Kuu Bara na kwenye mchezo dhidi ya Yanga aliweza kupambana vyema kwa kuweza kuwathibiti wapinzani wao.
Ulikuwa ni mchezo wake wa kwanza kucheza dhidi ya Yan­ga akiwa na jezi za Simba, lakini kiwango chake hakikuwa cha kubeza japo alikiona cha moto kutoka kwa beki mwenzake Yondani ambaye alimfanyia kitendo kibaya cha kumtemea mate.
SHOMARY KAPOMBE – SIMBA
Alisaidiana vema na Mkude katika nafasi ya kiungo wa kati. Kapombe na Mkude waliweza kuibeba zaidi Simba kwenye nafasi hiyo ambapo Kapombe aliyezoeleka kucheza beki wa kulia, alifanya kazi ya ziada kui­vuruga Yanga.
Credit to Global Publishers
MaoniMaoni Yako