Vijana Zanzibar kupewa Ruzuku


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea na azma yake ya kuwawezesha vijana kiuchumi ili waweze kujiajiri kutokana na rasilimali zilizopo katika nchi yao.
Akiwasilisha hutuba ya Bajeti ya Wizara ya vijana ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Balozi Ali Abeid Karume amesema mpaka sasa serikali imesha waandalia mazingira maalumu vijana ya kujikwamua na umaskini ikiwemo kuwaingizia ruzuku vijana katika mabaraza yao.
Amesema mbali na kuwaingizia ruzuku vijana katika mabaraza yao lakini pia watawapa mafunzo vijana juu ya shughuli za kilimo ,uvuvi na biashara ili waweze kujiari wenyewe.
Aidha amesema mafunzo hayo yatawawezesha vijana kujikwamua na umaskini na kuondokana na hali ngumu ya maisha ambayo inawakabili pamoja na kuimarisha Uchumi uliopo.
Aidha Balozi karume ametowa wito kwa Vijana kujiunga katika mabaraza ya Vijana ili waweze kunufaika na ruzuku zinazopatikana ambazo zitawasaidia kuanzisha miradi ya kujikwamua na umaskini.
Zaidi ya shilingi Bilioni 7 zimeombwa kuidhinishwa na Baraza la Wawakilishi ili ziweze kutumika katika matumizi ya kawaida ya wizara hiyo pamoja na kuimarisha miradi ya maendeleo katika mwaka wa fedha 2018/19.
MaoniMaoni Yako