VIDEO: Zari, ampa makavu Ringtone Apoko kisa kumuhonga Range Rover Sport


MPENZI wa zamani wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ amesema hamfahamu Ringtone Apoko ambaye ni msanii wa muziki wa Injili kutoka nchini Kenya aliyetangaza kumnunulia mrembo huyo gari aina ya Range Rover Sport.

Hapo jana Ringtone Apoko aliweka wazi kuwa amenunua gari hilo baada ya kusikia Zari atawasili nchini humo kwa ajili ya event yake, pia kipindi cha nyuma msanii huyo alipopata taarifa za Zari kuachana na Diamond alijitokeza na kueleza ana nia ya kumuoa


Sasa leo May 11, 2018 Zari akiwa nchini Kenya amehojiwa na kituo cha Radio, Kiss FM na kueleza kuwa hamfahamu msanii huyo.

“Simfahamu huyo Ringtone na sijawahi kukutana naye, ndio mara ya kwanza kusikia kitu kama hicho. Nina watu zaidi ya milioni 3.9 katika mtandao wa Instagram ambao wananifuatilia, siwezi kujua nani kunifuata na kwa wakati upi,” amesema Zari.

MaoniMaoni Yako