VIDEO: Nyota Simba wapiga shangwe la kufa mtu Dodoma


Dodoma. Ni nderemo na vifijo usiku wa leo hapa katika hotel ya Golden Crown  mahali ambapo Wachezaji wa Simba wameamsha bonge la Sherehe wakishangilia Ubingwa wa Ligi kuu bara ambao umetokana na kupoteza kwa wapinzani wao wakubwa Yanga.

Mwanaspoti kama ilivyo kawaida yake kukupatia  hatua kwa hatua limeshuhudia nderemo za wachezaji wa timu hiyo wakiongozwa na Mganda Emmanuel Okwi na Nahodha John Bocco bila lumsahau Shizza Kichuya wameonekana kufurahia vilivyo ubingwa huo ambao wameupata kabla ya mchezo wao na Singida United keshokutwa Jumamosi.

Licha ya kufanikiwa kuwa mabingwa lakini wachezaji wote wa Simba wameonyesha kuwa na ari kubwa ya kwenda kupambana dhidi ya Singida ili kulinda rekodi yao ya kutopoteza mchezo wowote msimu huu.

Credit: Mwanaspoti
MaoniMaoni Yako