Friday, May 4, 2018

VIDEO: Diego Costa Amstaafisha Vibaya Wenger…Arsenal Yaondolewa Europa


]AKIITU-MIKIA Arsenal kwa miaka 22 hatimaye ni rasmi Kocha Arsene Wenger amehitimisha safari ya kuinoa timu hiyo akiwa hana taji lolote la Ulaya baada ya kushuhudia timu yake ikifungwa bao 1-0 na kuondolewa katika nusu fainali ya Europa League.
Arsenal imepata kipigo hicho kutoka kwa Atletico Madrid ambapo ‘muuaji’ wao alikuwa ni Diego Costa, yuleyule ambaye alikuwa akiwasumbua walipokutana naye England alipokuwa akiichezea Chelsea.
Katika mchezo wa jana ukiwa ni nusu fainali ya pili kwenye Uwanja wa Wanda Metropolitan, Costa alifunga bao hilo katika dakika ya 45 akipokea pasi kutoka kwa Antoine Griezmann.
Matokeo hayo yameifanya Atletico ifuzu fainali kwa jumla ya mabao 2-1 kwa kuwa katika mchezo wa kwanza timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.
Atletico itakabiliana na mshindi wa kati ya Salzburg na Marseille, ambao mechi yao iliongezewa muda baada ya matokeo kuwa 2-2 hadi tunakwenda mtamboni jana.
Nahodha wa Arsenal, Laurent Koscielny aliumia kifundo cha mguu na kutolewa kwa machela dakika ya 12, hali ambayo inatia hofu juu ya ushiriki wake na timu ya taifa ya Ufaransa katika Kombe la Dunia mwezi ujao.
Atletico inawania kushinda taji hilo kwa mara ya tatu tangu ilipofanya hivyo mara ya mwisho mwaka 2012 ilipoifunga Athletic Bilbao mabao 3-0 kwenye fainali.
Fainali ya mwaka huu itapigwa Mei 16 kwenye Uwanja wa Parc Olympique Lyonnais wa Ufaransa.
Mafanikio pekee ya Ulaya kwa Wenger ambaye ataondoka klabuni mwishoni mwa msimu huu ni kucheza fainali ya Uefa Cup (2000) na Ligi ya Mabingwa (2006) ambapo zote alipoteza.

ATLETICO MADRID (4-4-2): Oblak 6.5; Thomas 7 (Savic 90+3), Gimenez 7.5, Godin 7.5, Lucas 6.5; Saul Niguez 6.5, Gabi 6.5, Koke 7, Vitolo 5.5 (Correa 74); Costa 8 (Torres 83), Griezmann 7.5
Subs not used: Gameiro, Filipe Luis, Olabe, Werner
Goals: Costa 45+2
Bookings: Gabi, Saul Niguez, Costa
Manager: Diego Simeone 7
ARSENAL (4-3-2-1): Ospina 6; Bellerin 5.5, Mustafi 6, Koscielny 5 (Chambers 12, 6.5), Monreal 6; Ramsey 6.5, Xhaka 5.5, Wilshere 7 (Mkhitaryan 68, 6); Welbeck 6.5, Ozil 6.5; Lacazette 6.5
Subs not used: Cech, Iwobi, Kolasinac, Maitland-Niles, Nketiah
Bookings: Wilshere, Monreal, Mustafi
Manager: Arsene Wenger 6.5
Referee: Gianluca Rocchi (Italy)

Chanzo: Global Publishers