Ukimya wangu ulisababishwa na msiba – Nisher

Mtayarishaji wa video za muziki, Nisher amefunguka kwa kuwaomba radhi mashabiki wake kutokana na ukimya wa mwezi mmoja ambao alikuwa nao.

Nisher amedai matatizo ya msiba wa babu yake yamesababisha ashindwe kufanya baadhi ya mambo pamoja na kukaa mbali na mashabiki wake.
Director huyo ameandika, “Siku 14 zilizo pita zimekua siku Ngumu sana kwangu na ninachukua nafasi hii kuwaomba radhi mashabik wangu na wadau wote mnao ni support nimeshindwa kabisa hata kupost wala kua karibu na simu yangu kutokana na kwamba Nilifiwa na Babu yangu mzaa baba (mwanzo KUSHOTO) ikanilazimu kuacha kila kitu nlichokua na fanya Dar (Maana mimi ni Mtoto wa Kwanza kwetu) na kuja Arusha Kwaajili yakua karibu na Familia lakini zaidi sana Baba Yangu (KATIKATI) Ambaye siku chache kabla ya birthday yake alifiwa na baba yake mzazi…. Hii imenigusa sana na Familia zetu pamoja na ndugu jamaa na marafiki wakaribu na imetukutanisha pamoja na kutufanya kua karibu zaidi katika kipindi hiki kigumu. Ijapokua Babu alifariki katika uzee mwema Bado tunazikumbuka Busara zake na Maneno yake ya Hekima na jinsi alivyo kua akipenda kila mtu awe na Umoja na Mshikamano. Tutakukumbuka sana Mzee wetu Lala kwa Amani. Naomba radhi sana Mashabik na wadau wangu wote kwa Delay zozote zilizo/zinazo/zitakazo jitokeza katika kipindi hiki kigumu, na nashukuru kwa privacy yenu pia.! #rip
Chanzo: Bongo 5

by richard@spoti.co.tz
MaoniMaoni Yako