Tetesi za usajili Ligi Kuu Tanzania bara leo Alhamis 24 May 2018


Imeripotiwa kuwa uongozi wa klabu ya Simba upo mbioni kuachana na Kocha wake Mkuu Mfaransa, Pierre Lechantre huku nafasi yake ikichukuliwa na Msaidizi, Mrundi, Masoud Djuma.
Klabu ya yanga sc na Singida United wanawania saini ya Mshambuliaji
Feisal Salum kutoka JKU ya visiwani Zanzibar.
Mbeya City wameonesha nia ya dhati ya kuhitaji huduma ya mshambuliaji wa timu ya Mwadui fc Awesu Awesu
Imeripotiwa kuwa Ditram Nchimbi yupo mbioni kuondoka Njombe Mji na kujiunga na klabu ya Mbao Fc ya Jijini Mwanza.
meripotiwa kuwa Hassan huenda akaikacha klabu ya Mtibwa Sugar na kujiunga na klabu ya Kagera Sugar.
Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Yanga sc zimetabainisha kuwa huenda ukaachana na mshambuliaji wake Amisi Tambwe.
Klabu ya Azam fc ipo mbioni kumsainisha mchezaji wa Ruvu Shooting Hamisi Mcha imeripotiwa kuwa mazungumzo yanakwenda vyema
Taarifa kutoka kwa watu wa karibu na mchezaji wa klabu Simba Sc wameweka wazi kuwa Mohamed Ibrahim Mo huenda akatimkia katika klabu ya Yanga sc
Pia Ibrahim Ajibu imeelezwa kuwa hana furaha katika klabu yake ya Yanga sc hivyo yupo tiyari kuvunja mkataba wake na klabu ya Singida United inamtolea macho
Hata hivyo Pappy Tshishimbi aweka wazi kuwa ataondoka katika klabu ya Yanga sc na kwenda kujiunga na klabu ya zesco
Pia klabu ya Simba Sc huenda ikumtupia vilango Salim Mbonde hii ni kutokana na kuandamwa na majeruhi ya mara kwa mara
Imearifiwa kwamba klabu ya Azam fc ipo tiyari kutoa ofa katika klabu ya Simba Sc ili kuweza kumsajili beki Paul Bukaba
Said Ndemla ameweka wazi kuwa hana mpango wa kuondoka katika klabu ya Simba Sc Pia Ndemla alihusishwa kutimkia klabu ya Yanga sc
MaoniMaoni Yako