Tetesi za Usajili Barani Ulaya Leo Jumatano 2/5/3018
Naibu mkufunzi wa Liverpool Zeljko Buvac anapigiwa upatu kumrithi mkufunzi wa Arsenal anayeondoka Arsene Wenger . (Pravda BL, via Mirror)

Arsenal huenda isimlipe mkufunzi wake mpya zaidi ya kitita cha £8.5m ambacho mkufunzi wake Arsene Wenger alikuwa akipata kwa mwaka (Daily Mail)

Beki wa Manchester United Eric Bailly, 24, ana wasiwasi kuhusu hatma yake katika klabu hiyo baada ya kutochezeshwa na mkufunzi wa klabu hiyo Jose Mourinho. (Mirror)

Mabeki Matteo Darmian na Daley Blind, wote wakiwa na umri wa 28 wameambiwa kwamba wako huru kuondoka klabu hiyo mwisho wa msimu huu. (Times)

Chelsea inamnyatia Anthony Martial, 22, iwapo Manchester United haiwezi kumrai raia huyo wa Ufaransa kusalia katika klabu hiyo ya Old Trafford (Telegraph)

Kiungo wa kati wa Roma Radja Nainggolan, 29, amepinga madai kwamba anahusishwa na uhamisho wa Chelsea na Manchester United kwa kuamua kusalia katika klabu hiyo ya Serie A. (Daily Mail)

Huenda wakufunzi wa Chelsea na Napoli Antonio Conte na Maurizio Sarri wakabadilishana vilabu.(mirror)

Ajenti wa kiungo wa kati wa Napoli Jorginho amethibitisha kwamba kumekuwa na hamu ya mchezaji huyo kutoka nje huku klabu za Manchester United na Manchester City . (Manchester Evening News)

Mshambuliaji Andy Carroll, 29, huenda asishirikishwe katika mechi muhimu ya West Ham dhidi ya Leicester siku ya Jumamosi baada ya mgogoro na meneja david Moyes katika mazoezi (Guardian)

Ross McCormack atapata takriban £1m kama nyongeza ya marupuru iwapo Astona Villa watapandishwa daraja hadi katika ligi ya Premier, licha ya kutocheza mechi hata moja msimu huu. (Sky Sports)

Beki wa Brazil David Luiz, 31 huenda akaelekea Napoli iwapo Rafael Benitez atarudi katika uwanja wa San Paolo kuchukua mahala pake Maurizio Sarri kama mkufunzi mwisho wa msimu huu. (Sun)

Kiungo wa kati wa zamani wa Liverpool Steven Gerrard ataweza kukabili shinikizo iwapo ataajiriwa kuwa mkufunzi mpya wa klabu ya Rangers , kulingana na mchezaji mwnza wa zamani Frank Lampard. (Talksport)

Kiungo wa kati Gerard Deulofeu, 24, amesema kuwa anaweza kuelekea Watfor kwa uhamisho wa kudumu baada ya kukiri kwamba hatma yake katika klabu ya Barcelona haijulikani.(Mundo Deportivo)
Chanzo: BBC
MaoniMaoni Yako