Tetesi Za soka Barani Ulaya Leo Juma tano 16/05/2018

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino yuko tayari kuwakataa Chelsea kwa sababu anasema ana furaha kuwa na klabu yake. (Star)

Arsenal wamefanya mazungumzo na kiungo wa kati wa Nice Jean-Michael, 26, ambaye thamani yake ni pauni milioni 40. Lakini mahasimu wao wa London Chelsea wanaongoza mbio na kumsaini raia huyo wa Ivory Coast. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Arsenal Mikel Arteta, 36 anakaribia kuwa meneja mpya wa Arsenal akichukua nafasi ya Arsene Wenger baada ya mazungumzo kuendelea kati ya pande hizo mbili. (Independent)
Nahodha wa zamani wa Arsenal Patrick Vieira, 41, anasema amekasirishwa mshahara ulionukuliwa na klabu hiyo baaada ya kuzungumziwa kuhusu nafasi ya umeneja iliyo wazi. (Sky Sports)
Manchester United wana uhakika wa kumsaini mlinzi Toby Alderweireld, 29, kutoka Tottenham. Red Devils wana nia ya kutumia pauni milioni 40 kwa mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Ubelgiji. (Evening Standard)
United pia wako kwenye mazungumzo ya kumsaini beki Matthew Bondswell, 16, kutoka Nottingham Forest. (Mail)
Mlinzi wa Leicester Harry Maguire, 25, hatma yake itaamuliwa baada ya mechi za kombe la dunia baada vilabu kadha vikuu vya Premier League kummezea mate mechezaji huyo wa kimataifa wa England. (Mirror)
Everton watahitaji kulipa pauni milioni 6 ikiwa watamfuta meneja Sam Allardyce. Meneja wa zamani wa Watford Marco Silva ndiye ana nafasi nzuri ya kuchukua wadhifa huko Goodison Park. (Express)
QPR watamateua meneja wa zamani wa England Steve McClaren kama meneja wao mpya kuchukua mahala pake Ian Holloway, ambaye alifutwa wiki iliyopita. (Sky Sports)
Kiungo wa kati wa Newcastle Jonjo Shelvey, 26, hatajumuishwa kwenye kikosi cha Uingereza kitakachoshiriki kombe la dunia kutokana rekodi yake mbaya kinidhamu. (Mirror)
Manchester United wako tayari kuilipa Napoli pauni milioni 44 kumpata beki Elseid Hysaj msimu huu. Raia huyo wa Albania wa umri wa miaka 24 atakuwa mlinzi namba saba ghalia zaidi duniani. (Sun)
Everton watamfuta meneja Sam Allardyce saa 48 zinazokuja na wanakaribia kumteua aliyekuwa meneja wa Watford Marco Silva. (Mirror)
Afisa mkuu mtendaji wa Arsenal Ivan Gazidis na mkrugeni mkuu Josh Kroenke wamemtambua kiungo wa kati wa zamani wa Arsenal Mikel Arteta ambaye sasa ni kocha huko Manchester City kama mtu anayeweza kuchukua mahala pake Arsene Wenger kama meneja wa Arsenal. (Mail)
Source:BBC Swahili
MaoniMaoni Yako