Tanzania yajitosa mashindano ya tenisi AfrikaArusha: Jumla ya wachezaji wanne wa timu ya tenisi wapo nchini Kenya kwenye mashindano ya vijana ya Afrika kusaka viwango vya ubora kwenye mashindano yanayofanyika kwa siku sita kuanzia Mei 28 hadi Juni 3.


Kocha aliyetanguzana na Kikosi hicho, Goodluck Mollel licha ya kuwa mara yake ya kwanza kuwa na kikosi hicho kilichokuwa chini ya Kocha Nicolaus Leringa anauhakika wa kufanya vyema kwenye mashindano hayo.


Wachezaji hao ni Kanuti Alagwa, Nicolas Mela, Debora Lema na Caroline Mwangata ambao watachuana kama mchezaji mmoja mmoja na pia kama timu ya wawili wawili.


Nchi zinazoshiriki katika mashindano hayo ni wenyeji Kenya, Tanzania, Burundi, Madagaska, Misri, Visiwa vya Shelisheli, Mauritius, Rwanda, Nigeria, Benini, Togo na Algeria.


Aliongeza kuwa katika michezo ya awali waliweza kupoteza dhidi ya Madagaska na Benini na juzi walishinda dhidi ya Kenya, Shelisheli, Benini na pia Madagaska katika mchezo wa pili.
MaoniMaoni Yako