Tamko la yanga baada ya kusikia ngoma kasaini azam


Na George  Mganga

Baada ya uongozi wa Azam FC kutangaza rasmi kuwa wameingia mkataba wa awali wa mwaka mmoja na Mzimbambwe, Donald Ngoma, uongozi wa Yanga umesema umesikitishwa zaidi na kitendo alichokifanya mchezaji huyo.

Ngoma aliyekuwa akiitumikia Yanga tangu mwaka 2015 hakuweza kucheza takribani mechi za msimu mzima unaomalizika hivi sasa (2017/18) kutokana na kuwa majeruhi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili na Usajili ndani ya Yanga, Hussein Nyika, amesema kuwa Ngoma hajafanya jambo la kiungwana na limemuumiza yeye kama kiongozi kwa kuamua kuondoka kimyakimya bila mawasiliano na uongozi wake.

"Naweza kusema Ngoma hajafanya kitendo cha kiungwana hata kidogo, nimeumizwa kwa kitendo chake cha kuondoka na kuhamia klabu nyingine, yote kwa yote namtakia kheri huko alipohamia" amesema Nyika.

Hiki karibuni uongozi wa Yanga kupitia Nyika ulisema utafanya maamuzi magumu kuhusiana na Ngoma kutokana na kukaa nje ya dimba kwa muda mrefu akisumbuliwa na majeraha.

Ngoma alisajiliwa na Yanga akitokea FC Platnumz ya nchini kwao Zimbambwe na kuweza moja ya wachezaji tegemeo ndani ya kikosi cha kwanza cha timu hiyo, na hii ni kutokana na umahiri wake aliokuwa akiuonesha ndani ya Uwanja.

Source: Saleh Jembe

MaoniMaoni Yako