Sugu kutinga bungeni kesho Kesho Jumatatu May 21

Siku 11 baada ya mbunge wa Mbeya, (Chadema) Joseph Mbilinyi maarufu ‘Sugu’ kuachiwa huru, kesho Mei 21, 2018 ataingia bungeni.
Sugu ataingia bungeni kuwawakilisha wananchi wa Mbeya baada ya kulikosa bunge hilo la bajeti tangu lilipoanza Aprili mwaka huu.
Sugu amesema: “Nipo Dodoma tayari, nimekuja baada ya hali ya mama yangu kuendelea kuimarika na kesho (Mei 21,2018) nitaanza kuwawakilisha wana Mbeya walionituma.”
“Wana Mbeya walikosa mwakilishi, walikosa wa kuwasemea mambo yao, kwani kilichotokea juu yangu ilikuwa kuwanyima fursa Mbeya kusikika ndani ya mjengo, sasa nimerudi kuwatumikia kwa nguvu zangu zote.”... Soma Zaidi
MaoniMaoni Yako