Sugu Atinga Bungeni kwa Mara ya Kwanza Taka Atoke Gerezani aibua Shangwe


Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi (Sugu) kwa tiketi ya CHADEMA, ameingia Bungeni na kusalimia baadhi ya Wabunge na kibua shangwe.

Leo Mei 21 Wabunge wameshangilia mbunge huyo kwa kwa kupiga makofi kwa muda wa nusu dakika huku Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge akitaka Wabunge kuacha kupiga makofi na kipindi cha maswali na majibu kiendelee.

Mbunge Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ aliachiwa huru kutoka gereza la Ruanda, Mbeya Mei 10 alipokuwa akitumikia kifungo cha miezi mitano.

Sugu alitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela February 26, 2018 kwa kutoa lugha ya fedhea dhidi ya Rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara walioufanya Desember 30, 2017 katika uwanja wa shule ya msingi Mwenge, Mbeya. 
Credit: Udaku Specially
MaoniMaoni Yako