Powered by Blogger.

Slider

Breaking

MICHEZO

HABARI

MAGAZETI

UDAKU

BURUDANI

VIDEOS

» » Steven Gerrard Awa Kocha Mkuu wa Timu hii kubwa Barani Ulaya


Steven Gerrard hatimaye amekabidhiwa Timu kama kocha wake mkuu na hivyo kuanza kazi ya kuinoa timu hiyoa Meneja wake. Ni Rangers ya Skotiland inayoshiriki katika ligi ya Scottish Premiership kwa mkataba wa miaka Minne 4.
“Ninajisikia furaha na heshima kubwa sana kuwa Kocha mkuu ajaye wa timu hii ya Rangers. Hakika hili siyo jambo dogo kamwe. Nina heshima kubwa kwa timu hii na utamaduni wake” Alisema Gerrard.
“siwezi kabisa kusubiria kuanza kufanya kazi hii kama kocha wa Rangers. Ninatarajia kuyajenga mafanikio makubwa katika klabu hii, hasa nikiendeleza pale nilipoikuta.” Aliongeza Gerrard.
Mwenyekiti wa Klabu hiyo alisema, “kutokea mwanzon I kabisa mwa mazungumzo yetu na Gerrard, mazungumzo yetu yamekuwa yenye mwitikio wa chanya kabisa na wenye dalili za kuzaa matunda. Na tunaamini kwamba Gerrard ndiye mtu sahihi wa kuichukua Rangers kutoka hapa na kuiendeleza kwa mafanikio makubwa zaidi” Alisema Dave King.
Gerrard ambaye uzoefu wake kama kocha ni ule alioupata tu alipokuwa anafundisha kikosi cha Wadogo Liverpool yaani Under 18, alikuwa ni Keptain mzuri na mwenye mafanikio katika siku zake kama mchezaji muhimu wa Liver.
Gerrard kama kocha wa Rangers anakibarua kizito hasa mbele ya timu bora kabisa zinazoshiriki ligi ya Scottish, mfano kama Celtic. Lakini Gerrard anaamini anatosha kusimama mbele ya nguli wa michezo ya mpira wa miguu kama kocha atakayekuwa na mafanikio akiwa na Rangers.


«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post