Wednesday, May 30, 2018

Singida united yashusha kifaa hichi toka Brazil

Tags


Klabu ya Singida United imeanza kuonesha juhudi za maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara kwa kumshusha Mbrazil, Felipe Oliveria dos Santos kutoka Brazil.

Santos amewasili Singida akiwa tayari ameshamalizana na timu hiyo iliyomaliza ligi msimu uliomalizika ikishika nafasi ya tano.Santos aliwahi kucheza soka lake katika klabu ya Asec Mimosa ya Ivory Coast vilevile akiweza kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mbrazili anakuwa wa pili kumwaga wino Singida United baada ya Faisal Salum kutoka JKU kutajwa pia kuwa tayari ameshasaini mkataba wa kuitumikia klabu hiyo.