Simba yawaharibia YangaDar es Salaam: Straika Mtogo wa Wolaitta Dicha, Arafat Djako ameanza mazungumzo na Simba ambayo inatumia mbinu za kisasa kuhakikisha inamnasa baada ya Yanga iliyoonyesha nia awali kutofanikisha usajili wake.


Djako ambaye amemaliza mkataba wake na Wolaitta Dicha, timu hizo za Kariakoo jijini Dar es Salaam, zimeonyesha nia ya kumuhitaji baada ya kuridhishwa na kiwango chake walipomwona kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Djako alikuwa kwenye kikosi cha Wolaitta kilichocheza na Yanga Dar es Salaam wakafungwa 2-0 na mchezo wao wa marudiano wa Ethiopia walishinda 1-0, bao lilifungwa na straika huyo aliyefuga rasta kichwani lakini walikuja kutolewa kwa tofauti ya mabao.


Habari za ndani ni kwamba, licha ya Yanga kuonyesha lengo hilo la kumsajili, sasa hivi Simba ndiyo wamekuja kwa kasi kuhakikisha hawafanyi makosa na kuinasa saini yake.


"Jamaa bado kidogo, mipango wanayoifanya ni moto, kuhakikisha wanamsajili mchezaji huyo lakini imekuwa ya siri sana,"amesema jamaa huyo.


Hata hivyo, Djako mwenyewe ameongeza kwa njia ya simu na kusema kama kutakuwa na jambo hilo watu watajulishwa kwani sasa ni mapema: "Nafiki kama kuna jambo lolote litajulikana tu kwa sasa hakuna kitu kama hicho, si kweli."
MaoniMaoni Yako