Simba Kukabidhiwa Ubingwa Mjini Singida.

Baada ya Simba kujihakikishia ubingwa wa VPL 2017/18 Haji Manara aliiomba bodi ya ligi kuwakabidhi kombe mara baada ya mchezo wao dhidi ya Singida United kwenye uwanja wa Namfua mkoani Sinqida.

lengo la Manara lilikuwa ni kupitisha kombe hilo kwenye baadhi ya mikoa wakati timu ikirejea Dar: Tutaandaa utaratibu mkubwa wa kufurahia kombe Singida na namna ya kulirudisha Dodoma, Morogoro mpanga Dar.”

Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi kuu Tanzania bara (TPLB) Boniface Wambura amesema hajapokea ombi lolote kutoka Simba wakitaka kukabidhiwa kombe uwanja wa Namfua Singida.

“Ombi la Simba kukabidhiwa kombe Singida mimi sina taarifa hiyo wala hawajawasiliana na bodi ya ligi, utaratibu wa kukabidhi kombe tutautangaza baada ya mechi ya kesho dhidi ya Singida United.


Source: Bbc

MaoniMaoni Yako